Wakazi katika Wilaya ya Kilindi wameshiriki katika siku ya Usafishaji Duniani ambayo huadhimishwa Septemba 20 ya kila mwaka.
Wakazi hao wameshiriki kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Barabara kuu ya Songe –Handeni
Akizungumza katika maadhimisho hayo Katibu Tawala Wilaya ya Kilindi ndugu Tamko Mohamed Ally alisema siku ya Usafishaji Duniani ni muhimu katika kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa kufanya usafi katika maeneo yao ili kujikinga na madhara mbalimbali yanayotokana na uchafuzi wa mazingiri
Alisema i usafi wa mazingira ukiimarishwa jamii itaepukana na magonjwa ya milipuko kama vile kuharisha na kutapika
Aliwataka wakazi wa wilaya ya Kilindi wanaoishi kandokando ya Barabara katika kipindi cha mvua wahakikishe wanapanda miti na kufanya usafi wa mazingira
Katibu Tawala Tamko aliwataka wananchi wa wilaya ya Kilindi kubadilika na kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi kwani Kilindi bila uchafu inawezekana
Kauli Mbiu ya siku ya Usafishaji Duniani mwaka 2025 ni “Tunza Mazingira kwa kuzipa Taka Thamani”
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.