Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mh:Hashim Mgandilwa amewataka vijana katika Wilaya ya Kilindi kujiepusha na makundi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuvuruga amani nchin na badala yake wawe walinzi wa amani katika maeneo yao
Akizungumza na vijana katika vijiwe vya vijana kuhamasisha na kuwaelimisha vijana na wananchi wengine kuilinda amani Mh:Mgandilwa aliwataka vijana kukataa kutumika kuharibu utulivu uliopo kwa maslahi ya watu wenye nia ovu na kuwataka kutoa taarifa katika vyombo husika kwa tukio au mtu yeyote anaehamasisha kuvunjka kwa amani
Sanjari na hayo Mkuu huyo wa wilaya aliwaagiza vijana wasio na leseni kujiorodhesha ili kunufaika na mafunzo ya udereva katika chuo VETA iliwaweze kukidhi kupata leseni na kunufaika na fursa ambazo zinatolewa na serikali ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ambapo vijana wametengewa asilimia 4
Alisema kwa kutambua changamoto za vijana Mh: Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameanzisha Wizara maalum ya vijana ili kurahisisha kutatua changamoto za vijana
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.