Watumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Kilindi wamehamasishwa na kuelimishwa umuhimu wa kuwekeza katika masoko ya Fedha na Hisa kwa ajili ya akiba na maendeleo
Akizungumza na watumishi katika ukumbi mdogo wa Halmashauri Afisa Masoko kutoka taasisi ya UTT AMIS ndugu Theresia Mrema alisema taasisi hiyo ya Serikali ilinzishwa ili kuwasaidia watanzania kuwekeza katika mifuko ya pamoja kwa lengo la kujiwekea Akiba kwa ajili ya maendeleo mbalimbali
Alisema kupitia mifuko ya UTT AMIS watanzania wanaweza kuwekeza kwa gharama ndogo ikiwemo shilingi 5000 na kuendelea kwani hata gharama za kuendesha mifuko hiyo chini ya UTT AMIS ni ndogo,usalama wa hakika za fedha na urahisi wa kuweka na kutoa fedha
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.