Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi ndugu John Mgalula amesema mapambano dhidi ya Saratani ya matiti hayana budi kuwalinda wanawake
Akizungumza wakati wa semina elekezi kuhusu uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti Mgalula alisema Saratani bado ni tatizo katika jamii hivyo mapambano ya kupambana na ugonjwa huo jamii hususani wanawake wapewe kipaumbele kwani wamekuwa waathirika wakubwa wa ugonjwa huo
Alilishukuru shirika la PFIZER FOUNDATION kwa kufikisha mradi huo katika Halmashauri ya wilaya ya Kilindi kwani utawanufaisha wananchi wengi
Naye Afisa ufundi kutoka mradi huo unaofadhiliwa na PFIZER FOUNDATION Dk Sunday Wanyika alisema mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri zote za mkoa wa Tanga
Washiriki wa semina hiyo walikuwa Viongozi wa dini,watumishi wakiwemo watendaji kata na maendeleo ya jamii na watu
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.