1.0 Utangulizi
Idara ya Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana ni kati ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi. Idara ina vitengo vya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana, ambapo majukumu yake ni kuratibu na kusimamia upatikanaji wa huduma za jamii na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi ya jamii. Katika utekelezaji wake Idara inaratibu mipango ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF - Tanzania Social Action Fund), Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF – Re-organized Community Health Fund), Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za Wanyonge wa Tanzania (MKURABITA), Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na Kuratibu asasi zisizokuwa za ki serikali (NGOs & CBOs) na vikundi vya kiuchumi.
2.0 Muundo na Rasilimali watu.
Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi ina vitengo vitatu, ambavyo ni kitengo cha Maendeleo ya Jamii, kitengo cha Ustawi wa Jamii na Kitengo cha Vijana.
3.0 Majukumu yanayotekelezwa na idara
Idara kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizopo utekeleza majukumu yake kwa mgawanyo unaozingatia taaluma na miundo ya serikali.
3.1 Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
3.2 Kitengo cha Ustawi wa Jamii
3.3 Kitengo cha Vijana
Kusaidia vijana kupata mbinu za kujiinua kiuchumi na kutambua fursa na vikwazo vilivyo katika mazingira yao na kujiletea maendeleo.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.