IDARA YA KILIMO NA USHIRIKA
-Kuratibu huduma za kilimo za ugani ili kuboresha uzalishaji na kuzuia uharibifu wa mazingira.
•Kushirikiana na wadau wa kilimo kuanzisha mashamba darasa.
•Kutoa taarifa mbalimbali kuhusu mazao ya kilimo na masoko.
•Kutunza takwimu za uzalishaji wa mazao ya kilimo.
•Kutoa taarifa kuhusu usalama wa chakula katika wilaya.
•Kuwafundisha wakulima kuhusu kilimo bora na mbinu bora za kuhifadhi mazao.
-Kuratibu shughuli za ushirika.
•Kukagua hesabu za vyama vya Ushirika.
•Kusimamia Mikutano Mikuu ya vyama vya Ushirika.
•Kusajili Vyama vya Ushirika.
•Kukusanya takwimu za biashara ya mazao ya kilimo katika vyama vya Ushirika.
KITENGO CHA USHIRIKA
1.0 UTANGULIZI
Ushirika ni kitengo ndani ya Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika. Nchini Tanzania Ushirika unaongozwa na Sheria ya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake za mwaka 2015. Ushirika huendeshwa katika misingi saba ya Ushirika inayotambulika duniani kote na kuzingatia maadili ya Ushirika ambayo yalipitishwa na Tamko la Muungano wa Vyama vya Ushirika Duniani (International Co-operative Alliance – ICA) maadili hayo ni; Uanachama wa Hiari na ulio wazi, udhibiti wa Kidemokrasia/kiutawala, Ushiriki wa wanachama katika shughuli za kiuchumi, Uhuru na kujitegemea, Elimu, mafunzo na taarifa, Ushirika miongoni mwa vyama vya ushirika na Ushirika kuijali jamii.
2.0 LENGO LA USHIRIKA
Lengo kuu la Ushirika ni kuinua kipato cha wanachama na jamii kwa ujumla, kuungana na kufanya kazi pamoja kwa hiari na kufanikisha mahitaji ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli inayomilikiwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia.
3.0 MAJUKUMU YA OFISI
Ofisi ya Ushirika inayo wajibu wa kutekeleza majukumu ya kisheria, usajili na kuwezesha udhibiti na usimamizi wa Vyama vya Ushirika katika Wilaya, ikiwa pamoja na kutekeleza majukumu yafuatayo;
4.0 AINA YA VYAMA VYA USHIRIKA VILIVYOPO WILAYANI KILINDI
Ushirika hutofautiana kutokana na mahitaji ya jamii husika, kuna aina mbalimbali za Ushirika kama vile Ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS), Ushirika wa mazao (AMCOS), Ushirika wa viwanda, Ushirika wa madini na nyingine nyingi kutegemeana na mfungamano “common bond” ya jamii husika. Kuna aina mbalimbali za ushirika hapa Wilayani Kilindi kama vile Ushirika wa kuweka na kukopa (SACCOS), Ushirika wa mazao (AMCOS), Ushirika wa viwanda na Ushirika wa madini.
4.1 Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS)
SACCOS zilizopo Wilaya ya Kilindi ni pamoja na Umoja SACCOS, Kwamwande SACCOS, Baraka SACCOS, Azimio Mafisa Madukani SACCOS, Vijana SACCOS, Negero SACCOS, Muungano SACCOS, Kimbe SACCOS, Jaila SACCOS, Msanja SACCOS, Mafulila SACCOS, Kikunde SACCOS, Kilindi SACCOS, Songe Ward SACCOS, Songe Farmers and Business SACCOS na Kwediboma SACCOS.
Madhumuni makubwa ya uwanzishwaji wa SACCOS hizo ni pamoja na :-
4.2 Ushirika wa Mazao (AMCOS)
AMCOS zilizopo wilayani Kilindi ni Nguu Farmers, Kilindi Farmers, Kilimo Mseto na Kingo Farmers.
Madhumuni ya uwanzishwaji wa vyama hivyo ni pamoja na:-
4.3 Ushirika wa Kiwanda
Wilaya ya Kilindi ina chama kimoja cha Ushirika wa Kiwanda ambacho kinaitwa Kilindi Industrial Co-operative, madhumuni yake ni pamoja na:-
4.4 Ushirika wa Madini
Vilevile, wilaya ya Kilindi ina jumla ya vyama viwili vya Madini ambavyo ni pamoja na Kiwaleke Mining Co-operative na Ngeze Mining Co-operative.
Madhumuni ya uwanzishwaji wake ni pamoja na:-
Imeandaliwa na,
Romana Milinga
KAIMU AFISA USHIRIKA (W)
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.