Wakazi Wilayani Kilindi wametakiwa kuongeza mwitikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh:Hashim Mgandilwa wakati alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo kiwilaya yalifanyika katika kijiji cha Msamvu katika kata ya Tunguli
Alisema ugonjwa wa Ukimwi bado ni tataizo na ndio maana kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwaka 2025 ni mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuendelea na mwitikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo
Akizungumzia kuhusu upimaji wa Virusi vya ukimwi Mh:Mgandilwa alisema bado kuna mwitikio mdogo wa kwenda kupima hususani wanaume wengi hawapendi kupima ili kuja afya zao na badala yake hutegemea vipimo kutokana na majibu ya wake zao pindi wanapokuwa wajawazito
Alisema wanaume wote waone umuhimu wa kwenda kupima na kutaja kuwa wilaya ina asilimia 0.9 ya maambukizi hali ambayo inaonyesha bado hali hii si nzuri na kutaka kuungwa mkono kwa jitihada za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.