Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa amesema serikali wilayani Kilindi itahakikisha watoto wanaoandikishwa shule na wanaofaulu kujiunga kidato cha kwanza wanapata haki yao ya elimu kwa maendeleo ya jamii na taifa
Mh Mgandilwa alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo kiwilaya yalifanyika katika kijiji na kata ya Kibirashi
Alisema inasikitisha kuona baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kilindi hawawapeleki watoto wao shule na wengine kuwaelekeza watoto wanapofanya mitihani ya kumaliza emu ya msingi wajifelishe ili wabaki nyumbani
Alisema kuanzia Januari serikali itahakikisha wazazi wote wenye watoto wanaotakiwa kuanza elimu ya msingi wanawaandikisha watoto hao shule na asiyefanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria
MhMgandilwa alisema serikali ya awamu ya sita imekuwa ikihakikisha inaboresha miundombinu ya elimu katika wilaya Kilindi ikiwemo kutoa fedha za ujenzi wa shule mbili mpya za msingi Mduguyu na Samia kupitia mradi wa BOOST na kuongeza katika mwaka 2003 Wilaya ya Kilindi ilikuwa na jumla ya shule za msingi 73 na sasa ina shule 128 za serikali na binafsi 5.
Alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha miundombinu ya shule kwa kuongeza vyumba vipya vya madarasa, kukarabati shule kongwe na ujenzi wa shule mpya ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu bora.
Mambo mablimbali yalifanyika kabla na wakati wa maadhimisho ikiwemo kupanda miti,kufanya usafi wa mazingira,midahalo na insha ambapo washindi wa insha walipatiwa zawadi mbalimbali.
Modi Mngumi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.