Tatizo a uharibifu wa vivuko vya vijiji vya Mgera kata ya Kisangasa na Ludewa kata ya Kikunde limepatiwa ufumubuzi baada ya serikali kutoa fedha kwa ajili ya matengenezo ya vivuko hivyo
Kaimu meneja wa TARURA wilayani Kilindi Mhandisi Gwamaka Mwaipaja amesema kupitia fedha za Mfuko wa barabara zaidi ya Tsh 56.7 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha miguu katika barabara ya Mgera sekondari kilichopo kata ya Kisangasa.
Mhandisi Mwaipaja amesema muda wa mkataba mradi wa matengenezo ya kivuko hicho ulianza 12/03/2022 na kukamilika tarehe 12/06/2022 ambapo wananchi kwa sasa wanakitumia kivuko hiki
Mradi mwingine uliokamilika ni matengenezo ya dharura kupitia fedha za Tozo ambapo zaidi ya Tsh milioni 33.19.Fedha hizo zimefanikisha matengenezo ya kivuko cha Ludewa kilichopo barabara ya Kikunde-Ludewa-Mnangali na kwamba ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.Matengenezo ya kivuko hiki yalianza tarehe 13/05/2022 na kukamilika tarehe 13/08/2022
MODI MNGUMI-KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.