Halmashsuri ya Wilaya ya Kilindi imekabidhi Pikipiki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao wa kazi za kila siku
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ndugu John Mgalula akiongea katika hafla ya kukabidhi Pikipiki hizo iliyofanyika Ofisi za makao makuu ya Halmashauri alisema Pikipiki hizo ni mwendelezo wa Halmashauri kuhakikisha inanunua vitendea kazi kwa Maafisa wake katika ngazi tofauti za Halmashauri ili kurahisisha utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo ya makabidhiano ambaye alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilindi Bibi Tamko mohamed Ally aliipongeza Halmashauri kwa kuwapatia maafisa hao vitendea kazi ambavyo vitawasaidia katika kazi zao ikiwemo kufuatila marejesho,kutembelea vikundi vya ujasiriamali na kuhamasisha jamii kushiriki kazi za maendeleo
Pikipiki hizo zimetolewa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata za Kimbe,Kilindi,Pagwi,Msanja,Saunyi,Songe
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.