Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 632 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Afya na Elimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wikaya ya Kilindi Ndugu John Mgalula alisema shilingi milioni 442 ni kwa ajili ya miradi ya Afya,shilingi milioni 140 Elimu sekondari na shilingi milioni 50 ni Elimu Msingi
Miradi ya Afya ni ujenzi wa kituo cha Afya Negero (Shilingi milino 250 ),maboma ya Zahanati ni Zahanati ya Kwediboma Juu (Shilingi milioni 60),Zahanti ya Kingo(Shilingi milioni 60),Zahanati ya Mmbogo (Shilingi milioni 12) na Zahanati ya Misufini (Shilingi milioni 60)
Alisema Upande wa Elimu sekondari kwa maboma ya vyumba vya maabara yaliyofikia hatua ya lenta ni Shule ya Kibirashi shilingi milioni 30,Kilindi shilingi milioni 30 na Negero shilingi milioni 30.
Maboma ya vyumba vya madarasa kwa upande wa Elimu sekondari yaliyofikia hatua ya lenta Mkurugenzi Mtendaji alisema ni Mafisa (shilingi milioni 25 na Seuta sekondari (Kwamba shule mpya ) shilingi milioni 25.
Elimu Msingi maboma ya vyumba vya madarasa yaliyofikia hatua ya lenta ni Tamota shilingi milioni 25 na Ndwati shilingi milioni 25.
Mkurugenzi Mtendaji alimshukuru Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa fedha hizo kwani zitawezesha miradi hiyo kutekelezwa ujenzi wake na wananchi kunufaika na huduma zake
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.