Tatizo la ukosefu wa zahanati katika vijiji sita wilayani Kilindi lapatiwa ufumbuzi kufuatia serikali kutoa shilingi milioni 300 za ukamilishaji zahanati zilizoanza kujengwa na wananchi
Fedha hizo tayari zimeshatumika kumalizia zahanati hizo sita ambazo zitakuwa ni ukombozi kwa wananchi kwa kuwaondolea kero ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma za matibabu maeneo ya jirani.
Serikali kuu ilitoa fedha hizo ambazo ziligawanywa kwa kila kijiji kupatiwa shilingi milioni hamsini ikiwa ni uungaji mkono nguvu za wananchi wake ambao wamekuwa wakitekeleza sera ya uchangiaji ujenzi kwa vitendo
Vijiji ambavyo vimejenga zahanati hizo ni Mabalanga ,Mnkonde,Kwamaligwa,Misufini,Mmbogo na Kwamfyomi.
Wananchi wa vijiji hivyo wameishukuru serikali kwani awali iliwalazimu kutembea umbali mrefu kati ya kilomita 5-10 ili kufuata huduma za afya na kuongeza kuwa hali ilikuwa mbaya zaidi kwa watoto na mama wajawazito
Walisema wanatoa shukrani zao za dhati kwani wanaona jinsi serikali yao inayohangaika kuhakikisha kero zao zinapatiwa ufumbuzi.
Sanjari na wananchi vingozi nao wakiongozwa na mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Abel Busalama nao walitoa shukrani kwa Mh:Rais kwa namna anavyohakikisha kero za wananchi na maendeleo ya nchi yanapatikana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Gracian Makota alisema serikali inayoongozwa na Mh:Dk Samia Suluhu Hassan inastahili pongezi za dhati kwa namna inavyotekeleza ahadi zake za kutatua changamoto za wananchi
Alisema miradi mingi inatekelezwa ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapiga hatua za kimaendeleo na kuboresha ustawi wa jamii.
MODI-MNGUMI-KILINDI
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.