Serikali kuu imetoa shilingi milioni hamsini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Kwamazuma iliyopo katika kijiji cha Kwamazuma kilichopo kata ya Kilindi.
Ujenzi wa nyumba hiyo ambayo ikiamilika itakuwa ni ya familia mbili ( 2 in one) na fedha za ujenzi wa nyumba hiyo zimetolewa na serikali kuu kupitia mradi wa EP4R
Serikali inayoongozwa na Mh:Dk Samia imedhamiria kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kwani fedha nyingi zimekuwa zikitolewa kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu,afya,barabara,maji ,umeme,uchumi.
Yote hayo yamekuwa yakifanyika ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za CCM kwa wananchi wake.Kilindi ni miongoni mwa wilaya ambayo imefaidika sana na miradi mbalimbali ya afya,elimu,maji,barabara,mifugo,kilimo,umeme.
MWISHO
MODI MNGUMI-KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.