Serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni mia moja kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe ya msingi Sangeni iliyopo kata ya Jaila katika Halmashauri ya wilaya Kilindi.
Akizungumzia ujenzi huo Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi Bwana Bahati Kahindi alisema fedha hizo zimetolewa na serikali kuu kupitia mradi wa EP4R
Alisema ukarabati katika shule hiyo kongwe utafanikisha kuirudisha shule hiyo katika hali nzuri na kuishukuru serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyotekelza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa vitendo
Bwana Kahindi alisema serikali imedhamiria kwa vitendo kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya ili wananchi wapate huduma bora kwa maslahi mapana ya jamii
Akizungumzia historia ya shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sangeni bwana Salimu Mbogo alisema Sangeni ni shule kongwe ambayo ilisajiliwa na serikali tarehe 01/07/1907
Alisema wanamshukuru Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyohakikisha miundombinu ya elimu inaboreshwa na kuwataka wazazi,walezi na jamii wanashirikiana na walimu katika kuhakikisha vijana wanazingatia masomo ili kuongeza ufaulu kwani watoto hao ndio taifa la kesho.
MWISHO
MODI MNGUMI-KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.