Serikali kuu kupitia mradi wa BOOST imeipatia Halmashauri ya wilaya Kilindi shilingi bilioni 1,512,500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya awali na msingi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Gracian Makota alisema fedha hizo zitaiwezesha Halmashauri kutatua tatizo la msongamano wa wananafunzi katika shule za Kibirashi na Mafisa
Alisema shule mbili mpya za mikondo miwili zitajengwa katika vijiji vya Mafisa na Kibirashi na kila shule itagharimu shilingi milioni 540,000,000/= na shilingi milioni 69,100,000/=zitajenga madarasa mawili ya elimu ya awali katika kijiji cha Kilindi ambayo yatakuwa ya kisasa yenye mahitaji muhimu kwa watoto.
“Hebu liangalie hili jambo na muujiza wake ambao unaikuta wilaya Kilindi unakwenda kupata mtu ambaye anakusaidia kuanzisha shule mpya ambayo haikuwepo na inaanzishwa na kuanza kufanya kazi”alisema Mkurugenzi Makota na kumshukuru Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha miundombinu ya elimu inakuwa bora
Mkurugenzi Makota alisema sanjari na hayo fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 2 na matundu 3 ya vyoo katika shule za msingi Jungu,Kwamngwaji,Mtonga na Mzinga ambapo kila shule itatumia shilingi milioni 56,300,000/=
Alisema shilingi milioni 137,600,000/= zitatumika kujenga vyumba 5 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Negero
Wananchi katika Halmashauri ya wilaya Kilindi wanatoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kuipatia Halmashauri fedha hizo ambazo zinaenda kutatua changamoto za kielimu
Ibara ya 80 ya Ilani ya CCM inaagiza serikali kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote
Modi Mngumi
Mawasiliano serikali Halmashauri ya wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.