Ofisi ya Mkuu wa wilaya Kilindi imemsaidia mtoto Chistosia Musa (13) kitimwendo chenye thamani ya shilingi 270,000/=
Kitimwendo hicho kimekabidhiwa tarehe 01/06/2023 kwa mtoto Christosia katika makao makuu ya Halmashauri na kushuhudiwa na viongozi wa Halmashauri na wilaya na watumishi mbalimbali
Akizungumza baada ya kukabidhi kitimwendo hicho Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Abel Busalama aliwataka wazazi na walezi wenye watoto walemavu wa aina yeyote kuhakikisha watoto hao wanapata malezi bora kama watoto wengine wasi na ulemavu
Alisema shule ya msingi Kwediboma ambayo ikikamilika ujenzi wake mtoto Christosia apelekwe shuleni hapo kwani shule hiyo inajengwa kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalum.
Naye baba mzazi wa Christosia mzee Musa Tumaina alisema mtoto wake alizaliwa akiwa na ulemavu huo ambao umesababisha kushindwa kumudu kutembea na kutoa shukrani kwa serikali kwa kusaidia kitimwendo hicho
Modi Mngumi
Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.