Shilingi milioni hamsini zimetolewa na serikali kuu kwa Halmashauri ya Wilaya Kilindi kwa ajili ya kutatua tatizo la upungufu wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Pagwi.
Fedha hizo tayari zimeanza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambayo ikiamilika itakuwa inaishi familia mbili za walimu(two in one)
Ujenzi huo ukikamilika utasaidia kutatua kero za walimu ikiwemo kukosa makazi bora ya walimu na familia zao.
Serikali kuu imekuwa ikitoa fedha mbalimbali kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo kujenga nyumba za walimu
Uongozi wa Halmashauri na wananchi wanatoa shukrani kwa serikali kwa namna inavyojitahidi kutatua kero za wananchi
MWISHO
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.