Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Batilda Buriani ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwa kuongoza katika ukusanyaji mapato kwa Mkoa wa Tanga, kwani hadi imefikisha asilimia 118 mwanzoni mwa mwezi Juni 2024.
“Napenda kuwapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwa kufikisha asilimia 118 ya mapato mwanzoni mwa mwezi Juni” alisema Bi. Batilda Buriani
Balozi Bi. Batilida ameyasema hayo alipokuwa katika kikao cha Baraza la Hoja Wilaya ya Kilindi kilichofanyika tarehe 14 Juni 2024 katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri.
Hata hivyo katika kikao hicho Bi. Batilda Buriani ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi chini ya Mwenyekiti Mhe. Idrisa Mgaza kwa namna ilivyo andaa mikakati ya kupunguza hoja za Mkaguzi wa Nje (CAG).
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mgaza amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji Ndg. John K.Mgalula kuandaa kikao maalumu cha Madiwani na wataalam kitakachotoa nafasi kwa madiwani kupitia hoja zote na majibu ikiwa ni pamoja na kutafuta suluhu ya hoja za miaka ya nyuma.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.