Kiasi cha fedha shilingi milioni 90 kilichotolewa na serikali kuu kimefanikisha kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba ya madaktari katika Halmashauri ya wilaya Kilindi
Nyumba hiyo ya madaktari imejengwa katika kijiji cha Mabombwe kilichopo katika kata ya Bokwa katika Halmashauri ya wilaya Kilindi
Nyumba hiyo ni pacha ambayo ina uwezo wa kuishi familia tatu( 3 in one)
Akizungumzia ujenzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya Kilindi Frank Herman alisema kukamilka kwa ujenzi huo kutapunguza tatizo la ukosefu wa nyumba za watumishi wilayani Kilindi.
Ameishukuru serikali inayoongozwa na na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassani kwa fedha nyingi ambazo imekuwa ikitoa kwa ajili kuboresha na kujenga miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi
Alisema Mh:Rais ametoa fedha nyingi za ujenzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya ikiwemo zahanati,vituo vya afya na hospitali.
MWISHO
MODI-MNGUMI-KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.