Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa tarehe 06/12/2023 akiwa pamoja na watumishi na wananchi wengine ameshiriki zoezi la kufanya usafi katika hospitali mpya ya Wilaya inayoendelea kujengwa katika Kijiji Cha Bokwa
Zoezi hilo la usafi ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara ambapo Wilaya imejipanga kufanya matukio mbalimbali ya usafi,utoaji elimu na upandaji miti
Kauli mbiu ya miaka 62 ya Uhuru mwaka 2023 kiwilaya inasema " Miaka 62 ya Uhuru,historian yetu,,amani yetu,tunza mazingira kwa Maendeleo endelevu"
Imetayarishwa Na. Modi Mngumi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.