Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndg Gracian Makota amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri fedha kiasi Cha Tshs 360 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 18
Akizungumza ofisini kwake amesema vyumba vitakavyojengwa ni kwa ajili ya wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza mwakani
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema ujenzi huo utaanza haraka ili kuhakikisha madarasa yanajengwa kwa wakati
Amesema Mh:Rais amekuwa akitoa fedha nyingi za miradi ili kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu
Amesema kwa namna ya kipekee anamshukuru Mh:Rais kwa namna anavyohakikisha elimu na Mambo mengine yanafanikiwa
Shule ambazo madarasa yatajengwa kupitia fedha hizo ni Kibirashi,Kikunde,Kimbe,Komkalakala,Kwediboma,Mafisa,Masagalu,Mbwego,Mkindi,Nkama na Pagwi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.