Halmashauri ya wilaya Kilindi imekamilisha ujenzi wa vyumba 18 vya madarasa katika shule za sekondari 11.
Ujenzi Wa vyumba hivyo umetekelezwa kufuatia serikali kuu kutoa fedha za ujenzi ikiwa ni mikakati ya serikali kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 hawakosi madarasa ya kusomea
Serikali kuu ilitoa kiasi cha Tsh milioni 360 kwa ajili ya ujenzi huo ili kupunguza tatizo la ukosefu wa vyumba vya madarasa.
Viongozi na wananchi wa Wilaya Kilindi wanatoa shukrani kwa serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo wilaya imekuwa ikinufaika na fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu.
Akizungumzia madarasa hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndugu Gracian Makota alisema anatoa shukrani kwa Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri fedha za vyumba hivyo 18
Alisema fedha hizo zimesaidia katika kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza hawakosi kwenda shule kwa sababu ya uhaba wa vyumba vya madarasa.
Alisema Halmashauri itahakikisha vijana wote waliochagaliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 wanaanza masomo na kumaliza lengo ni kuhakikisha vijana wanapata elimu kwa manufaa ya jamii na taifa.
Shule ambazo zilipata fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ni Pagwi,Kikunde,Nkama,Masagalu,Kwediboma,Mbwego,Kibirashi,Mafisa,Komkalakala,Mkindi na Kimbe.
MWISHO
MODI MNGUMI-KILINDI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.