• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kilindi District Council
Kilindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maendeleo ya Jamii
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Ardhi na Maliasili
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Shughuli za Mifugo na Uvuvi
    • Shughuri za Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu na Majukumu yake
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Mradi wa Maji
      • Miradi ya Afya
    • Miradi inayoendelea
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
    • Miradi iliyokamilika
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video Mbalimbali

JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA BINTI WA MIAKA 6

Posted on: April 22nd, 2021

Mahakama ya Wilaya Kilindi imemhukumu Elton Chrisopher (19) mkazi wa kijiji cha Kigwama kata ya Msanja kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka 6.

Hukumu hiyo ya kesi ya Jinai Na.97 ya mwaka 2020 imetolewa Aprili 13 mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Mariamu Mfanga

Akitoa hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi amesema mahakama imemhukumu mshtakiwa kifungo hicho baada ya upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha shtaka pasipo kuacha shaka yeyote.

Amesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka hilo kufuatia uthibitisho wa ushahidi uliotolewa na daktari  baada ya kumfanyia uchunguzi binti aliyebakwa pamoja na mashahidi waliofika kutoa ushahidi wakiwemo wazazi,walimu na majirani,ushahidi ambao haukuacha shaka yeyote.

Awali imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa polisi Koplo Sefu Makono kuwa mshtakiwa alimbaka binti huyo wa miaka 6 Oktoba 31 mwaka jana  katika kijiji  cha Kigwama kilichopo kata ya Msanja wilayani Kilindi.

Mwendesha mashtaka huyo ameendelea kudai kuwa mshtakiwa ambaye alikuwa ni mtumishi wa nyumbani kwa binti aliyembaka alimfanyia kitendo hicho baada ya kumpeleka katika nyumba mbovu iliyopo  karibu na nyumbani kwa mtoto huyo.

Koplo Sefu amedai kuwa binti huyo aligundulika amebakwa kufuatia jirani wa nyumba anayoishi mtoto huyo ambaye ni mwanamke kumuona binti huyo akiwa amelala na hakuwa akicheza na wenzake kama kawaida yake na alipomchunguza aligundua mtoto huyo akiwa na damu katika sehemu zake za siri.

Imeendelea kudaiwa kuwa baada ya tukio hilo taarifa ilitolewa polisi na mtoto alipelekwa hospitali ya wilaya Handeni ambapo vipimo vya daktari vilithibitisha kuwa binti alikuwa amebakwa.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi Mariam Mfanga ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya Kilindi kutoa ushirikiano pindi zinapojitokeza kesi kama hizo ili kukomesha vitendo vya ukatili  katika jamii.

MWISHO

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI KILINDI D-TANGA May 03, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA - SENSA 2022 May 05, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAKAZI WA WILAYA KILINDI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA

    September 15, 2021
  • WAKAZI WA KATA YA PAGWI WAANZISHA STOO YA MATOFALI

    August 07, 2021
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO HALMASHAURI YA WILAYA YA KILINDI YAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI

    August 05, 2021
  • JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA BINTI WA MIAKA 6

    April 22, 2021
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Seita
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Hati ya Mishahara
  • SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO TANZANIA, 2015
  • SERA YA TEHAMA YA TAIFA YA MWAKA 2016
  • SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTRONIKI YA MWAKA 2015
  • SHERIA YA MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI NA POSTA 2010
  • KITENGO CHA MUITIKIO WA DHARURA WA MATUKIO YA MITANDAONI
  • Mfumo wa Mpango na Bajeti
  • Mfumo wa ffars
  • Mwongozo wa Kutumia Mfumo wa FFARS

Tovuti Nyingine

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Baraza la Taifa la Elimu ya kiufundi
  • Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora
  • Tovuti ya Ikulu
  • TUME YA TAIFA YA UKIMWI TANZANIA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.