Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh:Hashim Mgandilwa amesema jamii inapaswa kutoa kipaumbele katika ulaji wa mlo kamili wenye makundi yote ya vyakula ili kuepukana na matatizo ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kukingwa kwa kuzingatia mlo sahihi
Akizungumza katika kikao cha robo cha tathmini ya lishe kilichofanyika tarehe 11/12/2024 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri Mh:Mgandilwa alisema serikali imekuwa ikihangaika sana katika kutibu watanzania wenye magonjwa ambayo yamekuwa yakisababishwa na mitindo ya maisha ya ulaji wa vyakula visivyozingatia mlo kamili
Alisema katika jamii ya sasa hata wakina mama hawapendi kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miaka miwili na kuwataka viongozi wa dini,mila na makundi mengine kutumia nafasi zao kuielimisha jamii kufahamau umuhimu wa watoto wadogo kunyonya kwa miaka miwili
Alisema kutokana na matatizo ya kutozingatia ulaji unaofaa hata vizazi vinavyozaliwa vinakuwa na upungufu katika uwezo wa kutafakari na mambo mengine ya kimaisha
Mh Mgandilwa alisema siku 1000 za mtoto zikijjumuisha miezi tisa na miaka miwili baada ya kuzaliwa ndio msingi wa kuzingatia lishe sahihi kwa mtoto kwani ndiyo inayomjenga katika uwezo wa akili na maarifa mengineyo.
Aliwataka watendaji kata kusimamia masuala ya lishe katika maeneo yao ya kazi kwa kuhakikisha kila shule inalima ekari sita za chakula ili angalau wanafunzi wapate mlo kwa siku wakiwa shuleni
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.