Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 429,720,000/= kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Songe ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuondoa kero za wananchi wake.
Akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Septemba 2022 Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Abel Yeji Busalama alisema mradi wa ujezi wa daraja hili ni miongoni mwa miradi iliyofanyika katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023.
Alisema ujenzi wa daraja la Songe umewezesha kutatua kero ya wananchi na wasafiri kushindwa kupita wakati wa mvua kubwa kwani maji wakati mwingine yanapozidi husababisha watu na vyombo vya usafiri kushindwa kupita hadi yapungue
Alisema serikali wilayani Kilindi inatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh:Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akitekeleza kwa vitendo ilani ya Chama kwa kutatua kero za wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara na kumtaja Mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Songe kuwa ni Motosach International
Akitaja mradi mwingine uliotekelezwa katika robo ya 2022/2023 Mh:Busalama alisema ni matengenezo ya barabara ya Songe Mjini kwa kiwango cha Lami (Mita 300),mradi uliotengewa kiasi cha shilingi 243,124,600/= unaotekelezwa na Mkandarasi JP Traders.
Akifafanua zaidi alisema miradi mingine ya ujezni wa miundombinu ni ujenzi wa daraja la Chamata (Lwande) ambao serikali ilitoa kiasi cha shilingi 984,870,500/= na Mkandarasi wa mradi huu ni Gloda Construction Co Ltd
Mradi mwingine uliotekelezwa katika robo ya kwanza ya 2022/2023 ni ujenzi wa daraja la Lusane kwenye barabara ya Tunguli (Msamvu)-Kibati ambao ulitengewa kiasi cha shilingi 124,000,000/=na kumtaja Mkandarasi wa mradi huu ni ATMO Constractors Ltd,na kuongeza kuwa miradi hii yote ya ujenzi wa miundombinu ilitekelezwa na TANROAD.
Akielezea miradi iliyotekelezwa na wakala wa barabara wa Vijijini na Mijini (TARURA) Mh:Busalama alisema wilaya imeendelea kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa kama ilivyoelekezwa katika ibara ya 56 ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Alisema TARURA wilayani Kilindi inahudumia jumla ya kilomita 871.59 na kwa mwaka 2021/2022 TARURA Kilindi ilipokea Tsh 1,038,153,784.47/= za Mfuko wa barabara (Road Fund),Tsh 500,000,000/=za mfuko wa jimbo (450,000,000/= zililetwa) na Tsh 1,000,000,000/= za Tozo (849,194,771.08 zililetwa)
Alisema katika mwaka wa fedha 2022/2023 TARURA Kilindi imepangiwa Tsh 980,113,478,.26/= za Mfuko wa barabara (Road Fund) na hadi mwisho war obo ya kwanza hapakuwa na fedha zilizopokelewa.
Mh:Busalama alisema ujenzi wa miundombinu ya barabara ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 ibara ya 55, ambayo imeiagiza serikali kuendeleza shughuli za ujenzi wa mindombinu mbalimbali na kuongeza kuwa utekelezaji wa miradi yote ya ujenzi wa miundombinu wilayani Kilindi ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na tatizo la ukosefu wa miundombunu kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo.
Akizungumzia huduma mbalimbali za kilimo zilizotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/2022Mh:Abel Yeji Busalama alisema jumla ya tani 33,840 za Mkonge ziligawiwa kwa wananchi wa kata za Msanja,Jaila na shule ya msingi Mgambo
Alisema lengo la kusambaza mbegu hizo ni ukinua kilimo cha Mkonge katika mkoa wa Tanga na hatimaye kuinua uchumi wa wananchi kupitia kilimo hicho.
Alisema sanjari na hilo serikali ilifanikwa kugawa kilo 2,397 za mbegu za Alizeti kwa wakazi wa kata za Bokwa,Kilwa na Msanja ambapo kwa zao la Maharagwe jumla ya kilo 2100 ziligawiwa katika kata za Kilindi,Pagwi,Songe,Bokwa,Mvungwe,Kibirashi na Masagalu
Akizungumzi sumu za viwavijeshi jumla ya lita 3648 zilitolewa na serikali kisha kugawiwa katika kata za Kwekivu,Tunguli,Lwande,Mabalanga,Kibirashi,Kilwa,Mkindi,Negero,Masagalu,Songe,Bokwa,Mvungwe,Kimbe,Msanja,Kisangasa,Kwediboma na Saunyi.
Mh:Busalama alisema zao la Korosho nalo halikuachwa kwani serikali katika mwaka 2021/2022 ilifanikiwa kutoa kilo 185 za mbegu na kuzigawa katika kata za Kilindi,Mvungwe,Kibirashi,Songe,Bokwa,Msanja na Mkindi na kwa zao la Mpunga serikali ilitoa kilo 1200 za mbegu na kuzigawa katika kata za Negero,Lwande,Kilindi,Kibirashi,Kilwa na Kimbe.
Mh:Busalama alisema ibara ya 37(B) (d) ya Ilani ya CCM inaagiza kuongeza uzalishaji na tija kwa mazao ya chakula na kuongeza utoshelevu wa chakula hivyo utoaji wa huduma zote katika kipindi cha utekelezaji kwa mwaka 2021/22 ni utekelezaji wa ilani ya chama kwa vitendo.
MWISHO
Na Modi Mngumi-Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.