Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya Kilindi limepitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi bilioni 32.1 kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025
Katika bajeti hiyo mapato kutoka mapato ya ndani ni shilingi bilioni 2.7
Sanjari na kupitisha bajeti hiyo pia baraza hilo limepitisha viapumbele vya bajeti hiyo kuwa ni kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani,kukarabati na kujenga miundombinu mipya ya afya na elimu na kumalizia miradi viporo,kutenga bajeti kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi za vijiji na kata
Kaimu Afisa Mipango katika Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Yudathadei Kway alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kutenga asilimia 10 kwa makundi ya wanawake,vijana na walemavu,lishe,kutekeleza ilani ya chama.
Vipaumbele vingine ni kuendelea na usimikaji wa mfumo wa kieletroniki wa usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za Afya (GoT-HoMIS) na kuongeza uzalishaji katika mazao ya chakula kwa usambazaji wa teknolojia sambamba na kuhamasisha matumizi ya mbegu bora
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.