Wilaya ya Kilindi imepanda jumla ya miti 1,975,000 ikiwa ni sawa na asilimia 131.66 ukilinganisha na lengo la Kitaifa la kupanda miti 1,500,000 kwa kila Wilaya kwa mwaka 2017/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo ameyasema hayo alipo kuwa akizindua wiki ya upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Uzinduzi huo umefanyika katika shule ya Msingi Kwamwande iliyopo ndani ya kata ya Bokwa.
Aidha katika kutekeleza hayo Wilaya ya Kilindi iliweka lengo la kupanda miti 1,983,000 ili kuhakikisha inarejesha uoto wa asili kwa haraka, hata hivyo miti yote ilipandwa lakini kulingana na changamoto mbalimbali miti 1,975,000 pekee ndiyo iliyomea ikiwa ni sawa na asilimia 99.6 kwa malengo ya Wilaya.
Hivyo mkuu wa Wilaya aliwapongeza viongozi wa vijiji, kata na Wilaya kwa utekelezaji wa agizo hilo. Nakuwasihi waendelee kuhakikisha wanatunza mazingira na kudhibiti vitendo vyote vya uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukata miti hovyo.
Kwa mwaka 2018/2019 Wilaya ya Kilindi imeweka lengo la kupanda jumla ya miti 1,959,000. Hivyo Mhe. Mtondoo amewataka viongozi wa vijiji kutunga na kusimamia sheria ndogo zitakazo hakikisha kila kaya inapanda miti isiyopungua mitano, lakini pia maeneo ya taasisi ikiwa ni pamoja na Shule na Zahanati zilizopo katika kila kijiji.
“Watendaji wote wa kata mhakikishe mnatoa taarifa za utekelezaji kabla ya tarehe 25.06.2019” alisema hayo Mhe. Mtondoo alipokuwa akisisitiza umuhimu wa wananchi kutunza mazingira yanayowazunguka kwa kupanda miti.
Naye Diwani wa Kata ya Bokwa Mhe. Idrisa Mgaza ameushukuru uongozi wa Wilaya kwa kufanya uzinduzi huo katika shule ya Msingi Kwamwnde ambapo zaidi ya miti 1500 inatazamiwa kupandwa katika shule hiyo.
Lakini pia wananchi wa kijiji cha Kwamwande hawakusita kuonyesha furaha yao kwa uongozi wa Wilaya kwa kushiriki zoezi la upandaji wa Miti katika Shule hiyo, hayo yalibainika pale Mzee Ibrahim Chauya alipopewa nafasi ya kuzungumza.
Imetayarishwa na.
Samwel D.Mwantona ( Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mheshimiwa Sauda S.Mtondoo akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande waliojitokeza katika uzinduzi wa Wiki ya upandaji Miti Wilaya. Uzinduzi huo umefanyika shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019. Ambapo jumla ya miti 1,959,000 inatarajiwa kupandwa ndani ya Wilaya ya Kilindi.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndg. Natus Manumbu akizungumza neno wakati wa maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ndg. Edward Masona akipanda mti katika shule ya Msingi Kwamwande, Siku ya uzinduzi wa wiki ya upandaji Miti Wilaya ya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo (katikati) akifuatilia uwasilishaji wa mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa uzinduzi wa juma la upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Wengine katika picha ni Diwani wa Kata ya Bokwa Mhe. Idrisa Mgaza (kulia kwake) na Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri Ndg. Edward Masona (kushoto kwake). Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande na Wananchi walioshiriki uzinduzi wa juma la upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kilindi Ndg. Clovis Mrutu akielezea faida za upandaji miti mara baada ya kupanda mti huo katika shule ya Msingi Kwamwande siku ya uzinduzi wa juma la upandaji miti Wilaya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Mwananchi kutoka kijiji cha Kwamwande akishiriki zoezi la upandaji miti kwa kupanda mti katika Shule ya Msingi Kwamwande siku ya uzinduzi wa juma la upandaji miti. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Baadhi ya wazee wa kijiji cha Kwamwande wakishirikiana kupanda mti katika uzinduzi wa juma la upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Diwani wa Kata ya Bokwa Mhe. Idrisa Mgaza akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa juma la upandaji miti Wilaya ya Kilindi. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Wanafunzi wakionyesha furaha yao mara baada ya miti kupandwa katika shule yao siku ya uzinduzi wa juma la upandaji Miti Wilaya ya Kilindi, huku Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo (aliyesimama nyuma mwenye ushungi mwekundu) pamoja na baadhi ya viongozi wakishuhudia tendo hilo. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Kwamwande leo tarehe 22.05.2019.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.