• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kilindi District Council
Kilindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maendeleo ya Jamii
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Ardhi na Maliasili
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Shughuli za Mifugo na Uvuvi
    • Shughuri za Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu na Majukumu yake
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Mradi wa Maji
      • Miradi ya Afya
    • Miradi inayoendelea
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
    • Miradi iliyokamilika
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video Mbalimbali

MHE. DC KILINDI "ZINGATIENI USAFI WA MAZINGIRA ILI KUPAMBANA NA MALARIA"

Posted on: January 16th, 2021

Wananchi katika wilaya Kilindi wametakiwa kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira ikiwa ni moja ya afua zinazosaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ukisababisha athari za kiafya na vifo kwa watanzania.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Sauda Mtondoo wakati alipokuwa akizindua zoezi la kitaifa la ugawaji wa vyanadarua katika ngazi ya kaya ambalo kiwilaya limefanyika katika kijiji cha Kwekivu.

Alisema ugonjwa wa Malaria umekuwa ukileta athari nyingi kiafya ambazo zimekuwa zikisababisha serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia matibabu na ununuzi wa dawa kwa ajili ya tiba kwa wananchi.

Mh:Mtondoo alisema viongozi wa serikali za vijiji vyote wilayani hapa kwa kushirikiana na wananchi wake wanatakiwa kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha kila mwananchi anazingatia kanuni za usafi kwa kusafisha mazingira yanayomzunguuka ili kutokomeza mazalia ya Mbu waenezao Malaria.

Akiizungumzia kauli mbiu ya kampeni ya kupambana na Malaria inayosema kabla hujalala chandarua ni lazima Mh:Mtondoo alisema haitakuwa na maana kugawa vyandarua kisha visitumike ipasavyo,hivyo wananchi wote wanapaswa kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hii kwa kuhakikisha wanatumia vyandarua wakati wote wa kulala.

Aliishukuru serikali awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli  kwa kuhakikisha inalinda afya za wananchi wake kwa kuendesha zoezi maalum la ugawaji wa vyandarua katika ngazi ya kaya na kuongeza kuwa uamuzi wa serikali wa kuwekeza katika kinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria ni wa muhimu na kusisitiza matumizi sahihi ya vyanadarua hivyo.

Alitoa onyo kwa wananchi ambao watatumia vyandarua hivyo kinyume na inavyotarajiwa kama vile kufugia vifaranga na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wananchi hao kwani serikali imetumia fedha nyingi kununua vyandarua hivyo

Zoezi la ugawaji wa vyanadarua ngazi ya kaya katika Wilaya Kilindi limezinduliwa kwa Mh:Mkuu wa wilaya kugawa vyandarua 15 katika makundi ya walemavu,wajawazito,watoto na wazee.

Zaidi ya kaya 80,000 zinatarajiwa kupata vyandarua katika zoezi linalotarajiwa kuendeshwa wilaya nzima ya Kilindi.

Habari Na: Modi Mngumi

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI WILAYA YA KILINDI KWAAJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2024 September 16, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA JESHI LA MAGEREZA February 01, 2024
  • TANGAZO LA CHAGUZI NDOGO ZA UDIWANI KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZA (NEC) February 17, 2024
  • TAASISI YA MO DEWJI KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA MACHO NA KUMUONA DAKTARI BINGWA WA AKINA MAMA BURE WILAYANI KILINDI June 23, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KILINDI YAPOKEA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 632 ZA MIRADI

    June 22, 2025
  • MRADI WA MAJI KWAMALIGWA-GITU KUNUFAISHA WAKAZI 36,263

    June 17, 2025
  • MWENGE WA UHURU WILAYANI KILINDI WAPITIA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 7.9

    June 10, 2025
  • MH: WAZIRI ULEGA AFANYA ZIARA NA KUKAGUA UJENZI WA BARABARA WILAYA KILINDI

    January 05, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Seita
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Hati ya Mishahara
  • SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO TANZANIA, 2015
  • SERA YA TEHAMA YA TAIFA YA MWAKA 2016
  • SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTRONIKI YA MWAKA 2015
  • SHERIA YA MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI NA POSTA 2010
  • KITENGO CHA MUITIKIO WA DHARURA WA MATUKIO YA MITANDAONI
  • Mfumo wa Mpango na Bajeti
  • Mfumo wa ffars
  • Mwongozo wa Kutumia Mfumo wa FFARS

Tovuti Nyingine

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Baraza la Taifa la Elimu ya kiufundi
  • Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora
  • Tovuti ya Ikulu
  • TUME YA TAIFA YA UKIMWI TANZANIA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.