Waziri wa Ujenzi Mh:. Abdalah Ulega amefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Handeni - Mafuleta inayojengwa kwa kiwango cha lami km 20 za awamu ya kwanza.
Waziri Ulega alifanya ziara hiyo tarehe 03/01/2025 na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mafuleta kilichopo katika kata ya Jaila
Mh:Ulega katika mkutano huo aliwaambia wananchi wa Wilaya ya Kilindi kuendelea kuwa wavumilivu na kumuunga mkono Mh. Rais Dk Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali na kuahidi kuipa kipaumbele barabara hiyo kwa kuhakikisha Mkandarasi anapata fedha kwa kadri zitakavyotolewa na Serikali ili kumuwezesha kukamilisha mradi huo.
Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Handeni - Kibirashi - Singida kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya Tsh. Bilioni 25 baada ya kuongezeka kwa muda wa mkataba.
Akitoa salamu za chama Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilindi Mh:Mohamed Kumbi alisema kukosekana kwa barabara bora zinazounganisha Wilaya ya Kilindi na wilaya za jirani sambambaba na barabara za vijijini zinazosimamiwa na TARURA kunaleta dosari na kufifisha mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita.
Hata hivyo amemhakikishia Mh. Waziri kuwa bado Wananchi wa wilaya ya Kilindi wanamshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa wanatambua kazi kubwa anayoendelea kuifanya Kilindi hususani katika Ujenzi wa miradi mbalimbali ya Elimu, Afya, Maji na Umeme.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kilindi ndg Tamko Mohamed Ally Katibu Tawala wa Wilaya amemshukuru Mh. Waziri kwa kutembelea mradi huo huku akimhakikishia kuwa wananchi wa Kilindi wataendelea kuwa wavumilivu kwa kuwa wanatambua juhudi za Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha WanaKilindi na Watanzania kwa ujumla wanawekewa mazingira mazuri ya kujikwamua kiuchumi.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.