Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.9
Miradi iliyopitiwa na mwenge huo tarehe 07.06.2025 katika wilaya ya Kilindi ni ujenzi wa vyumba vitatau vya madarasa na vyoo matundu sita,mradi wa kiuchumi nyumba ya kulala wageni,kikundi cha vijana bodaboda.
Miradi mingine ni ujenzi wa ofisi ya kata ya Kisangasa,mradi wa maji Kwamaligwa,ujenzi wa zahanati ya Kwamwande na ujenzi wa barabara ya lami Stendi kwa madoti Km 0.28
Akizungumza mara baada ya kukagua,kuzindua na kuweka jiwe la msingi,Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 ndugu Ismail Ali Ussi aliipongeza wilaya ya Kilindi kwa usimamizi mzuri wa miradi
Kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 inasema"Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025 kwa amani na utulivu"
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.