Tatizo la ukosefu wa kivuko kwa wakazi wa kijiji cha Mgera limepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kutoa zaidi ya Tsh milioni 56.7 kwa ajili ya matengenezo ya kivuko cha miguu katika barabara ya Mgera sekondari kilichopo kata ya Kisangasa.
Kaimu meneja wa TARURA wilayani Kilindi Mhandisi Gwamaka Mwaipaja alisema fedha zilizotumika kutengeneza kivuko hicho ni kutoka Mfuko wa Barabara (Road Fund)
Amesema muda wa mkataba mradi wa matengenezo ya kivuko ulianza tarehe 12/03/2022 na umekamilika tarehe 12/06/2022 na wananchi kwa sasa wanakitumia kivuko hicho cha miguu
Mhandisi Mwaipaja alisema kivuko hicho kimekuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa kijiji cha Mgera ambao awali walikuwa wakipata tabu kupita hasa wanafunzi na wagonjwa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mgera waliishukuru serikali kwa kutoa fedha za matengenezo ya kivuko cha sasa ambacho kinawawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali za maisha yao ya kila siku
Mwisho
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.