Katibu Tawala wilaya Kilindi Bibi Tamko Mohamed Ally amesema suala la watoto kupata chakula shuleni si hiari ni lazima na kuwataka watendaji kata kufuatilia suala hilo katika maeneo yao ili kuhakikiksha kila mtoto anapata chakula shuleni
Akizungumza katika kikao cha kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe robo ya pili kuanzia Oktoba hadi Disemba 2023,katibu Tamko alisema suala la chakula shuleni ni sera inayopaswa kutekelezwa bila kukosa na kila shule ilipewa agizo na Baraza la Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha kila shule inalima ekari 6 za chakula ili kuwa na uhakika wa chakula kwa wananfunzi
“Wanafunzi watafaulu vipi huku wakiwa na na njaa”?alihoji katibu tawala Tamko na kuongeza kuwa anahitaji taarifa ya kila shule ili kujua namna utekelezaji wa mpango wa chakula shuleni unavyotekelezwa hasa katika kipindi hiki cha kilimo na mtendaji wa kata atakaeshindwa kutekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua kali
Alisema watendaji wa kata wasimamie watendaji wa vijiji,walimu wakuu na wakuu wa shule na wasikae kimya na kuagiza anataka kupata taarifa za shule zote ambazo hazitoi chakula na kuongeza kuwa mojawapo ya sababu ya utoro wa watoto shuleni katika wilaya Kilindi ni ukosefu wa chakula kwani wapo ambao wanatembea umbali mrefu kuja shuleni bila kula chakula.
Alisema Watendaji wa kata na vijiji sio kwa ajili ya masuala ya ardhi tu hata masuala mengine ya maendeleo kama hayo ya watoto shuleni kupata chakula ni sehemu ya wajibu wao kwani ndio wasaidizi wakuu wa viongozi wa juu katika wilaya
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya kilindi Mh:Idrisa Mgaza akizungumza katika kikao hicho alisema agizo la madiwani kwa kila shule kulima ekari 6 za chakula ni lazima litekelezwe na wao kama wasimamizi wa masuala ya kimaendeleo katika halmashauri watafuatilia kila shule kuona utekezaji wa agizo walilolitoa
Alisema lengo la kuwa na uhakika wa chakula ni kuhakikisha Wilaya Kilindi watoto wake wanapata chakula shuleni kwani haina maana wilaya kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula katika mkoa huku wanafunzi shuleni hawana chakula na kuwa watoro kwa sababu ya njaa
Modi Mngumi
Kilindi DC
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.