Wakulima katika wilaya Kilindi wametakiwa kulima zao la Pamba ili kuongeza tija na kipato katika familia zao
Wito huo umetolewa na Balozi wa zao la Pamba Ndugu Aggrey Mwanri wakati alipokuwa katika ziara ya kuelimisha na kuhamasiha kilimo cha Pamba katika Halmashauri ya wilaya Kilindi
Alisema katika kubadili mtizamo na kuongeza tija wakulima wasikae na kutegemea mazao yaliyozoeleka kama vile Maharagwe,Mahindi na Alizeti ambayo yanatumika kwa chakula na biashara
Alisema zao la Pamba lenyewe ni zao la biashara ambapo kama wakulima watalima angalau ekari moja basi watakuwa na uhakika wa kuhifadhi mazao mengine kwa ajili ya chakula na kuitumia Pamba kuiuza kwa ajili ya biashara na hivyo kuweza kujiwekea akiba ya chakula
Alisema serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufufua zao la Pamba kwani mkulima atakaelima Pamba atakuwa na uhakika wa kupatiwa mbegu bora,dawa za kuua wadudu ,mabomba ya kupuliziza dawa na mwisho serikali kupitia bodi ya Pamba Tanzania itanunua zao hilo
Alisema uwepo wa fursa hizi zote ambazo serikali imepanga kuwapatia wananchi wake ni hatua nzuri katika kuwavutia wakulima kwani watakuwa na uhakika wa kila kitu kuanzia ulimaji hadi soko na kuwataka wanakilindi kubadilika na kuanza kulima zao la Pamba
Balozi Mwanri alisema zao la Pamba halihitaji mvua za kitimtim kama vile mazao ya Mpunga na Miwa bali zao hilo linahitaji mvua za wastani na ndio maana katika wilaya Kilindi Pamba inastawi kwa sababu ya hali ya hewa nzuri inayoruhusu kuzalisha zao hilo
Akiwa katika ziara hiyo Balozi Mwanri alitembelea na kuongea na wananchi katika kata za Masagalu,Kibirashi,Mabalanga,Jaila na Msanja
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.