Vituo vya huduma za afya katika Halmashauri ya wilaya Kilindi vimeondokana na tatizo la uhaba wa mashine za kupimia shinikizo la damu
Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya Kilindi Mariam A.Samiji alisema tatizo la upungufu mkubwa wa mashine hizo limeondoka baada ya serikali kuvipatia vituo 34 mashine 9 kila kimoja ambapo kituo cha Afya Songe kimepatiwa mashine 13 na kufanya jumla ya vituo kuwa 35
Wakizungumzia mashine hizo wataalam wa afya katika Halmashauri ya wilaya Kilindi walisema wanaishukuru serikali kwa kusaidia kutatua tatizp la uhaba wa mashine hizo muhimu katika kupima mapigo ya moyo ya wagonjwa na mama wajawazito
Walitoa shukrani kwa MhRais Dk Samia Suluhu Hassan kwa serikali yake anayoiongoza kwa kuhakikisha kero za ukosefu wa vifaa mbalimbali vya tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya zinatatuliwa
Modi Mngumi-Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.