Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe.Sauda Mtondoo leo amepokea mabati na Komputa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22.7 kutoka ofisi ya Mkugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano Tanzania na Banki ya ABC.
Misaada hii imetokana na juhudi iliyofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilindi chini ya Mhe.Sauda Mtondoo kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Gracian Makota kutembelea wadau mbalimbali wa maendeleo jijini Dar es Salaam ili kusaidia wananchi wa Wilaya ya Kilindi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kwa Watumishi wa Serikali Benki ya ABC Ndg. Emmanuel Nzutu alipokuwa akikabidhi mabati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6.7 kwaajili ya kuezeka maboma ya shule za Sekondari, alisema “kwakuunga mkono Serikali ya awamu ya tano kuhusu sera ya Elimu bure leo tunatoa mabati 200 kwa Wilaya ya Kilindi”.
Aidha mbali na mabati hayo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano Tanzania wametoa kompyuta 15 zenye thamani ya zaidi ya milioni 16 kwa uongozi wa Wilaya ya Kilindi kwa juhudi wanazozifanya, katika kuwaletea wananchi maendeleo.
“ Kompyuta hizi tutazitoa kwa shule ambazo zimefanya vizuri kwa upande wa elimu msingi lakini pia upande wa Sekondari” Alisema Mhe. Mtondoo alipokuwa akikabidhi kompyuta hizo kwa ungozi wa shule zilizofanya vizuri katika mitihani yao mwaka 2018 .
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mussa Semdoe alitoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Wilaya kwa juhudi mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea wana Kilindi maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Mtondoo na Katibu Tawala Wilaya Bi.Warda Maulidi kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Gracian Makota wamekuwa mstari wa mbele katika kuwatembelea wananchi na kukusanya kero zinazo wakabiri kisha kuziandalia mipango madhubuti ya kuzitatua kero hizo.
Ziara hii ya mafanikio ni moja ya mikakati iliyowekwa kwa lengo la kutatua kero ya mawasiliano kwa kwa vijiji visivyo na mawasiliano, ambapo vijiji vyote vimeisha ingizwa kwenye mpango wa kuunganishwa na na huduma ya mawasiliano. Pili ziara hii ililenga kutatua changamoto zinazokabili sekta ya Elimu wilayani.
Wahenga walisema mnyonge mnyongeni ila haki yake Mpeni. Hakika Viongozi wetu tunawapeni Hongera kwa kutekeleza Sera ya awamu ya tano kwavitendo.
Imeandaliwa na.
Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo (kulia) akiukabidhi uongozi wa Shule ya Msingi Boma, moja kati ya Kompyuta zilizotolewa na Mfuko wa Mawasiliano Tanzania. Walipokwa katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kwa Watumishi wa Serikali Benki ya ABC Ndg. Emmanuel Nzutu (Kulia) akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe.Sauda Mtondoo moja kati ya mabati 200 yenye thamani zaidi ya milioni 6.7 waliyoyatoa leo tarehe 20/03/2019 katika hafla fupi iliyoandaliwa Wilayani Kilindi.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.