Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya Kilindi imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo kwa serikali kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi
Akizungumza wakati akitoa maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa alimpongeza Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya chama
Alisem Dk Samia amekuwa akitoa fedha nyingi za kuboresha sekta ya elimu,afya,maji,umeme na nyinginezo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo
Alitao mfano wilaya Kilindi imepokea zaidi ya shilingi bil 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya elimu ya sekondari ambayo ikikamilika itainua ari kwa wakazi wa Kilindi kuwa na moyo wa kujiendeleza zaidi kielimu haswa kwa watoto wao
Mradi mwingine ni ujenzi wa kituo kikubwa cha umeme katika kijiji cha Kwamwande ambao ukikamilika utaondoa kabisa kero ya ukosefu wa umeme katika wilaya na kuinua zaidi shughuli za kiuchumi ikiwemo uchimbaji wa madini
Ujenzi wa hospitali ya wilaya na zahanati katika baadhi ya vijiji umelenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na maeneo yao ,sanjari na ujenzi wa mradi mkubwa maji wa Diburuma ambao ukikamilika,wakazi wengi wa wilaya Kilindi watakuwa na uhakika wa huduma ya maji wakati wote
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.