Katika kuhakikisha shughuli za ujasiriamali zinaendelezwa na kuimarishwa Halmashauri ya wilaya Kilindi imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 569,850,000.00 kwa vikundi 98 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu
Mikopo hiyo inatokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilindi kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Katika vikundi 98 vilivyopatiwa mikopo vikundi vya wanawake ni 54 ambavyo vilipatiwa mikopo yenye thamani ya 274,850,000.00, vijana vikundi 41 ambavyo vimepata mikopo ya shilingi milioni 280,000,000.00 na walemavu vikundi 03 shilingi milioni 15,000,000.00
Akizungumza katika hafla ya utoaji mikopo hiyo iliyofanyika tarehe 18 Novemba 2024 katika kata ya Kikunde Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi ndugu Chrispin Mng’anya alivitaka vikundi vilivyopata mikopo hiyo kuhakikisha wanarejesha kwa mujibu wa mikataba ili vikundi vingine vikopeshwe.
Naye Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Kilindi Bi. Ndayahundwa Bilama alisema kuwa mikopo hiyo imetolewa baada ya kusimamishwa kwa muda kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo marejesho kutorejeshwa ipasavyo.
Alisema kurejeshwa tena kwa mikopo hiyo ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kukopeshwa na kujiimarisha kiuchumi na kwamba kila kikundi kinapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa taratibu,kanuni na miongozo ya mikopo hiyo.
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.