Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa amewataka wakazi wilayani hapa kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura tarehe 27/11/2024
Mh Mgandilwa ametoa wito huo wakati alipokwa akizungumza na wanachi katika maeneo mbalimbali wilayani hapa katika mikutano ya kuelimisha na kuhamasisha watu kujiandikisha
Alisema trehe 27/11/2024 watanzania watashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuwachagua viongozi wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji na wajumbe wa halmashauri za vijiji
Alisema kila mtanzania aliye na umri wa miaka 18 anayo haki ya kikatiba ya kujiandikisha na kuwapigia kura viongozi anaowataka kwa ajili ya maendeleo katika maeneo yao
Zoezi la uandikishaji lilianza tarehe 11/10/2024 na linahitimishwa tarehe 20/10/2024
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.