Baraza la Waheshimiwa Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi wameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kuwashirikisha madiwani katika kutafuta ufumbuzi wa kutatua tatizo la ubovu wa Barabara za Kilindi ili kuhakikisha miundombinu hiyo inapatiwa fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wake
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi Mwenyekiti wa Baraza hilo Mh Idirsa Mgaza alisema Wilaya Kilindi ina tatizo kubwa la ubovu Barabara hata na wao kama Waheshimiwa Madiwani ni jukumu lao kuisemea Halmashauri katika vikao na kwingineko ili changamoto ya Barabara isikike na kupatiwa ufumbuzi kwa kutengewa fedha za kutosha
Alisema Waheshima Madiwani kwa niaba ya wanachi wao wanatoa shukrani kubwa kwa Mh Rais Dk Samia Suluhu Hasssan kwa kuipatia fedha Halmashauri ambazo zimewezesha kuboresha huduma za kijamii kama vile elimu na afya na kwa sasa kero kubwa ambayo inasumbua Halmashauri ni ubovu wa Barabara
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji kazi za TARURA katika kipindi cha Robo ya Tatu 2023/2024 Kaimu Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya Kilindi Mhandisi Gwamaka Mwaipaja alisema mpaka kufikia sasa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 robo ya tatu tarehe 30 Machi,2024 kiasi cha fedha kilichopokelewa kutoka Mfuko wa Barabara (Road Fund) ni Shilingi 257,617,641.10 kati ya shilingi 980,113,478.26 zilizopangwa ,ambapo kiasi kilichopokelewa ni sawa na asilimia 26.28 ya fedha zote zilizopangwa.
Alisema fedha za tozo zilizopokelewa ni shilingi 30,033,946.96 na kutaja changamoto ambazo TARURA katika Halmashauri ya Wilaya Kilindi inakumbana nazo kuwa ni jiografia ya Wilaya Kilindi barabara nyingi hupita katika milima na mabonde makubwa hivyo zinahitajio matengenezo makubwa pamoja na ujenzi wa madaraja
Changamoto nyingine ni uharaibifu wa vivuko vya barabara za Msente-Sangeni,Kwediswati-Saunyi na Tamota-Kwadundwa-Lulago-Lwande kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na uhaba wa maeneo ya kucimba changarawe/moramu kwa ajil ya ujenzi wa barabara
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.