Tatizo la ukosefu wa bwalo la chakula katika sekondari ya wasichana Kilindi limepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kuu kutoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo
Akizungumza ofisini kwake kuhusu fedha hizo Afisa Elimu sekondari wilaya Kilindi ndg Ntuli A.Mwakabungu amesema ujenzi wa bwalo hilo katika shule hiyo ya bweni ni mikakati ya serikali kuhakikisha miundombinu ya elimu inajengwa ili kuboresha mazingira ya elimu wilayani Kilindi
Amesema ujenzi wa bwalo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba,2022
Bwana Mwakabungu amesema idara ya elimu sekondari kwa namna ya kipekee inatoa shukrani kwa Mh: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa bwalo hilo
Amesema tayari mchanga,saruji,mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi vimeshawekwa eneo la mradi
Pia amesema serikali kuu imetoa kiasi kingine Cha fedha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Pagwi
Amesema ujenzi wa nyumba hiyo pia unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba,2022
Amesema ujenzi wa nyumba hii ambayo itatumiwa na walimu 2 itapunguza tatizo la ukosefu wa nyumba hizo na kulingana na mahitaji shule itakuwa na inahitaji nyumba 8 na kutoa shukrani kwa serikali kusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa nyumba za walimu
Shule ya sekondari Pagwi kwa sasa ina wanafuzi 286 na walimu 11
Modi Mngumi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.