Modi Mngumi-Kilindi
Shule ya sekondari Vibaoni iliyopo kata ya Tunguli katika kijiji cha Msamvu katika Halmashauri ya Wilaya Kilindi imepatiwa kiasi cha shilingi milioni 114 kwa ajili ya kutatua tatizo la ukosefu wa nyumba za walimu shuleni hapo
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi kaimu Afisa Mipango Ndugu Bahati Kahindi alisema fedha hizo zinatumika kujengea nyumba mbili za watumishi ambapo kila moja itaishi familia mbili hivyo kwa fedha hizo familia nne zitakuwa zimeondokana na tatizo la ukosefu wa nyumba za kuishi
Alitoa shukrani kwa serikali inayoongozwa na Mh:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyotatua kero za sekta ya elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya kufundishia na makazi ya walimu
Alisema Halmashauri ya Wilaya Kilindi imepokea fedha nyingi za kuboresha elimu ikiwemo kujenga nyumba za walimu,madarasa,ofisi,vyoo na kutengeneza samani mbalimbali
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.