Serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupitia Chama cha Mapinduzi yafanikisha kutatua tatizo la ukosefu wa kituo cha Afya katika kata ya Msanja iliyopo Halmashauri ya Wilaya Kilindi
Kero hiyo imetatuliwa kufuatia uamuzi wa serikali kutoa shilingi milioni 500 za ujenzi wa kituo cha Afya ambacho kitakuwa mkombozi kwa kusogeza huduma za matibabu ikiwemo upasuaji haswa kwa mama wajazito ambao inawalazimu kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za upasuaji pale inapohitajika
Wakizungumzia ujenzi huo wakazi wa kata ya Msanja walitoa shukrani kwa serikali kwa kuiona shida yao na kuipatia ufumbuzi
Walisema serikali ya awamu ya sita imefanya mengi katika kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ikiwemo kutoa fedha za umaliziaji wa zahanati kama vile Kwamfyomi,Mabalanga na Misufini.
Wakazi wa kata ya Msanja huwalazimu kusafiri umbali wa kilomita28 kufuata huduma za upasuaji wilayani Handeni au kilomita 98 kuja makao ya wilaya Kilindi Songe .
Modi Mngumi
Mawasiliano Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.