Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 wakagua uendelevu wa miradi, wazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2
Miradi ilyowekewa jiwe la msingi ni ujenzi wa zahanati kijiji Cha Kwamwande,barabara ya lami stendi Madoti km 0.28, mradi wa maji Mafulila/Bokwa
Mradi uliozinduliwa ni ujenzi wa chumba kimoja Cha darasa katika shule ya msingi Mswaki
Miradi ilyotembelewa ni mradi wa Vijana wa Bodaboda wa Kilindi Cha wagosi wa ndima Kwediboma na mradi wa kiuchumi wa shamba la miti Kwamaligwa
Sanjari na hayo Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 pia ulitembelea kitengo Cha watoto wenye uhitaji maalum shule ya msingi Kwediboma na kugawa viti mwendo 4 kwa watoto walemavu,Televishine na Surbuffer kwa ajili ya watoto hao kujifunza
Akizungumza katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio hizo kitaifa mwaka 2024 ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava alipongeza kwa uendelevu wa miradi,usimamizi mzuri wa miradi na kujali makundi yenye mahitaji maalum
Alitoa wito kuhakikisha miradi inakamilshwa na kutoa huduma bora kwa wananchi
Akizungumzia kuhusu ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka 2024 alisema kila Mtanzania anawajibu wa kulinda na kuhifadhi mazingira na kuhakikisha anashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi oktoba 2024
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge mwaka 2024 inasema tunza mazingira shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Maendeleo endelevu ya taifa
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.