Wilaya Kilindi ni moja ya wilaya iliyojumuishwa katika mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(Land Tenure Improvement Programe-LTIP).Mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unatekelezwa katika vijiji 83 ambavyo haikuwa na mpango wa matumizi bora ya Ardhi.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya kupokea mradi huu katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Kilindi,Afisa Ardhi katika wilaya Kilindi bwana Natus Manumbu alisema kikosi kazi maalum katika mradi huu kwa awamu ya kwanza kilianza kazi 18/12/2023
Alisema kila mwezi vijiji 10 vinatakiwa kuandaliwa mipango ya ya matumizi ya Ardhi na mpaka sasa vijiji 13 vimekamilisha na kuidhinisha mipango ya matumizi ya Ardhi
Afisa Manumbu alisema mradi unatekelezwa katika awamu mbili ambapo ya kwanza inahusisha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji husika na awamu ya pili itahusu upimaji na utoaji wa Haki za Hatimiliki za Kimila (CCRO’S) na kuongeza kuwa Haki za Hatimiliki za Kimila zitatolewa kwa wananchi na maeneo ya taasisi zilizopo vijijini.
Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Kwamba,Mvungwe,Vilindwa,Sambu,Mheza,Masagalu,Kigunga,Kwekivu,Mapanga,Ngeze,Mafisa,Mafisa Madukani na Lwande.
Aliizataja faida za mradi wa LTIP kuwa ni kuwezesha kutatua migogogro ya mipaka na matumizi ya vipande vya ardhi,uhifadhi endelevu wa mazingira,kuwezesha wananchi kumiliki vipande vya ardhi kwa mujibu wa sheria,kuwezesha wananchi kukopesheka katika taasisi za fedha.
Faida nyingine ni mirathi kumilikishwaa kwa warithi halali,wananchi na serikali kujikita katika shughuli za kimaendeleo na kuwa na mipango yenye tija kwa miundombinu na maendeleo mengine
Baadhi ya wananchi wakiuzungumzia mradi huu waliishukuru serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwani mradi huu utasaidia kuimarisha amani na utulivu kwa kuondoa migogoro ya ardhi na pia kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa kuwawezesha wananchi hasa wa vijijini kuweza kuwa na hatimiliki za kisheria na kuwa na uwezo wa kukopa
MODI MNGUMI
KILINDI DC
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.