Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S. Mtondoo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Lishe ya Wilaya kuhakikisha wanandaa Mipango ya Lishe Bora ili kupambana na matatizo ya Lishe wilayani
Mhe. Sauda S. Mtondoo ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizindua kamati ya lishe ya wilaya katika hafla fupi iliyo fanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi
Alisema ukosefu wa lishe bora unasababisha matatizo ya kiafya kwa watoto, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha hivyo aliitaka kamati kuhamasisha na kutoa elimu ya lishe bora kwa familia, jamii na wananchi wa Wilaya ya Kilindi katika ngazi zote za halmashauri
“Matatizo mbalimbali ya lishe yanaendelea kudumaza, kulemaza na hata kusababisha vifo vya watoto na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha”Alisema Mhe.Mkuu wa Wilaya.
Mhe.Mkuu wa wilaya alisema kuzinduliwa kwa kamati ya Lishe ya Wilaya ni utekelezaji wa Mpango mkakati wa serikali kuhusu lishe kwa wananchi kitaifa wa miaka mitano (National Multi sectoral Nutrition Action Plan) ulioanzia mwaka 2016 na utaishia 2021.
“serikali iliagiza kila Halmashauri kuunda Kamati za Lishe ngazi ya wilaya ambazo zinazohusisha wadau kutoka Idara mbali mbali, Mashirika ya Dini, taasisi za Elimu na Sekta Binafsi ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika kupambana na matatizo ya lishe” Alisema Mhe.Mkuu wa Wilaya
Mpango Mkakati wa Lishe wa serikali unajumuisha wataalam wa kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri pamoja na wadau wasio watumishi kama Viongozi wa mashirika ya Kidini na Sekta Binafsi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.