Kikao cha Wadau wa Elimu Wilaya ya Kilindi kilicho fanyika tarehe 15.04.2019 katika ukumbi wa Halmashauri kimejadili changamoto zinazo ikabili sekta ya Elimu ndani ya Wilaya ya Kilindi na kuweka mikakati ya kuzikabili changamoto hizo ili kuinua ufaulu wa wanafunzi.
Katika kikao hicho Mgeni rasmi Bi. Warda Maulidi ambaye ni katibu tawala wa Wilaya ya Kilindi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilindi alifungua kikao na kupokea taarifa zinazohusu Elimu ndani ya Wilaya ikiwa nipamoja na taarifa ya Kikao cha Mwaka 2018.
" Kila mjumbe atapata fursa ya kuchangia mikakati inayoweza ikanusuru Sekta ya Elimu ndani ya Wilaya yetu" alisema Bi. Warda Maulidi alipokuwa akifungua kikao hicho.
Mkakati wa kwanza ni kuhakikisha miundombinu ya shule yaani majengo na thamani za shule zinakamilishwa kupitia wadau ushirikianoo wa wadau lakini pia kuhamsisha jamii kutambua wajibu wao.
Akizungumza Mhe. Ndali Madoti, diwani wa kata ya Songe alisisitiza kuongeza juhudi za kusimamia wananchi kwa karibu ilikufanikisha ujenzi wa madarasa na kuondokana na tatizo la miundombinu katika shule zetu.
Hata hivyo Mkakati wa pili ulikuwa ni namna ya kudhibiti utoro wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na baraza la madiwani kutunga sheeria ndogo zitakazo saidiaa kudhibiti utoro wa wanafunzi, lakini pia kuhakikisha wazazi wanachangia upatikanaji wa chakula .
Hata hivyo wajumbe waliandaaa mkakati wa kukabiliana na tatizo la mimba mashuleni kwa kuunda kamati maalumu itakayohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwanasheria, Baraza la Madiwani na Walimu. Katika kusimamia hilo baraza la madiwani limehitajika kutunga sheria ndogo ya kuweza kudhibiti tatizo hili ikiwa nipamoja na kutoa Elimu kwa wazazi na walezi.
Aidha Mkakati wa nne ni upimaji na uwekaji alama katika maeneo yote ya shule ili kupunguza migogoro ya mipaka ya viwanja baina ya maeneo ya taasisi na jamii inayozunguka, katika kuhakikisha hili linafanikiwa Idara ya Ardhi imepewajuku la kusimamia mkakati huu.
Mkakati wa tano nikuelimisha jamii juu ya Sera ya Elimu bure ili waweze tambua wajibu wao kama wadau lakini pia mkakati wa sita kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata chakula shuleni ili kuongeza hari na kuweza kutoa masomo ya ziada.
Mbali na hivyo wajumbe walipitisha mkakati wa nane wa kuhakikisha mwajiri ahakikishe anaboresha maslahi ya Waalimu kwa kuwapa stahiki zao na Madeni wanayodai ili kuwaongezea hamasa ya kufanya kazi. Na ili kuhakikisha wanafunzi wote wanajua kusoma na kuandika wajumbe walipitisha Mkakati wa tisa wenye lengo maalumu kwa wanafunzi kuhusu Kujua Kusoma na Kuandika (KKK).
Mkakati mwingine ni kuboresha ikama ya walimu katika shule ili kuweza kuinua kiwango cha elimu na mwisho ni mkakati wa kuweka kambi za masomo kwa kuunganisha wanafunzi wa kata zilizojirani ili kuweza kutatua changamoto ya walimu wa masomo ya Sayansi. Na ili kufanikisha mkakati huu Walimu, Waratibu kata na Idara ya Elimu zimehitajika kusimamia zoezi hili.
Kikao hicho kilichoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda mtondoo, kilihusisha kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Idara ya Elimu, Walimu, Mashirika Binafsi, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kata na Vijiji, Wazazi na Wanafunzi.
Mbali na kikao hicho wanafunzi waliweza kuonyesha mambo mbalimbali yanayotokana na elimu wanayoipa shuleni. Wanafunzi wa Shule za Sekondari walionyesha namna ya kuandaa gesi ya Hydrogen pamoja na matumizi ya gesi hiyo kwa vitendo, lakini pia walionyesha namna ya kutengeneza sabuni pamoja na upimaji wa Tindikali (acid) na Alikali (bases) katika vyakula mbalimbali.
Imeandaliwa na:
Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Katibu Tawala Wilaya ya Kilindi Bi. Warda Maulid akizunguza jambo wakati wa kikao cha wadau wa Elimu Wilaya ya Kilindi kilichofanyika jana tarehe 15.04.2019 katika ukumbi wa Halmashauri. Katika kikao hicho Bi. Warda Maulid alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo aliyekuwa Mgeni rasmi.
Wanafunzi wa Sekondari ya Seuta wakionyesha mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutengeneza gesi ya Hydrogen lakini pia matumizi yake kwa vitendo. Kazi hiyo ilifanyika ukumbi wa Halmashauri wakati wa Kikao cha wadau wa Elimu siku ya tarehe 15.04.2019.
Katibu tawala wa Wilaya ya Kilindi Bi. Warda Maulidi akikagua maonyesho ya wanafunzi wa sekondari ya Seuta. Zoezi hili lilifanyika siku ya kikao cha Wadau wa Elimu Wilaya ya Kilindi, kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri siku yatarehe 15.04.2019.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha wadau wa Elimu wilaya ya Kilindi waliohudhuria kikao cha kujaidili mikakati ya Kuinua kiwango cha Elimu. Kikao hiiki kilifanyika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 15.04.2019
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ndg. Edward Masona akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau wa Elimu siku ya tarehe 15.04.2019. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.
Diwani wa Kata ya Bokwa Mhe. Idrisa Mgaza akielezea jambo wakati wa kikao cha Wadau wa Elimu Wilaya ya Kilindi, kilicholenga kutatua kero na changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 15.04.2019.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.