Mkurugenzi wa kampuni ya JSB ENVI-Dep LTD Bi.Saada Juma wa kwanza kulia katika picha akiwa na Ndg.Mgisha Pastori wa pili kulia na Afisa Usafi na Mazingira wa wilaya ya Kilindi Ndg.Winston Temba wa kwanza kutoka kushoto wakiwa katika Kikao cha tathmini ya athari za mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi africa mashariki (East africa crude oil pipeline-EACOP), Linalotarajia kupitishwa katika halmashauri ya wilaya ya kilindi.
Tathmini ya athari ya mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Afrika mashariki unaanzia kutoka kwenye eneo la ugunduzi lililopo kusini mwa ziwa Albertine nchini Uganda hadi rasi ya chongoleani iliyopo kasikazini mwa bandari ya Tanga Tanzania kwa ajili ya kusafirisha nje kwenye soko la kimataifa.
Wataalamu elekezi toka kampuni ya JSB Envi-Dep LTD ya kufanya tathmini ya athari ya mazingira na jamii zinazoweza kusababishwa na mradi pendekezwa walieleza kwakina juu ya mradi utakavyotekelezwa hatua kwa hatua kwa wajumbe wa kikao kutoka Ofisi ya Mkuu(W) kilindi ambayo pia ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Kilindi, Viongozi wa kata ambazo bomba la mafuta litapitia pamoja na wadau wengine.
Wataalamu wa JSB ENVI-Dep LTD waliwaelekeza wajumbe wa kikao kuwa ukiachana na jinsi mradi utakavyo tekelezwa kuna faida zake pia ambazo ni Kutoa ajira na fursa za biashara kama kutengeneza ajira za muda mfupi (miaka 2-3) na kutoa mafunzo kwa wenyeji, kusaidia mahudhui na manunuzi ya ndani
Pili kushiriki katika programu za maendeleo kama usalama barabarani na kujenga uwezo na Faida ya mwisho ni kuimarisha miundombinu kama vile barabara.
Pia watalaam hao walitoa furusa kwa wajumbe kutoa maoni, kuuliza maswali, mapendekezo na masuala yote yanayohusiana na mradi ili yaweze kuzingatiwa kwenye mchakato wa tathmini ya athari za mali na kubainisha njia za kupunguza ili kuhakikisha mradi unaendelezwa bila ya kusababisha athari kwa mazingira ya jamiii.
Watalaam walitaja kata ambazo bomba la mafuta ghafi litapitia kwa wilaya ya Kilindi kuwa ni Kibirashi, Kisangasa, na Mkindi. Lakini pia walisema pia katika kijiji cha Gitu kilichopo kata ya Kibirashi itajengwa kambi kubwa yenye uwezo wa kubeba wafanyakazi 1000 pamoja na kuhifadhi vifaa kwaajili ya ujenzi huu.
Aidha watalamu elekezi kutoka kampuni ya JSB ENVI-DEP LTD waliwataka viongozi ngazi za kata ambao bomba litapitia kubainisha shughuli za maendeleo zinazofanyika kwenye maeneo yao pamoja na vitu vinavyopatikana mfano maeneo ya matambiko, makaburi, misitu ya asili mabwawa n.k, ambapo vitu muhimu vilivyobainishwa ni Maeneo ya Shule, Maeneo ya Madini kama vile Kijiji cha Kinkwembe kilichopo kata ya Mkindi, Mashamba ya Kilimo na malisho ya mifugo, Malambo ya Maji na Bwawa la Maji la Kwamaligwa lililopo kata ya Kibirashi na Misitu ya Hifadhi ya eneo liitwalo Java.
Vingine ni maeneo ya watu binafsi na maeneo ya hifadhi za vijiji na kata.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.