Wajumbe wa kamati ya fedha,uongozi na mipango katika Halmashauri ya wilaya Kilindi wametembela mradi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kwamwande na kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi walioanza ujenzi huo kwa nguvu zao
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 04/05/2024 ikiwa ni mojawapo ya majukumu ya kamati hiyo kukagua miradi na kujionea maendeleo yake ili kujiridhisha na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi Mh:Idrisa Mgaza alisema wameridhishwa na ujenzi lakini ipo haja ya kuongezwa mafundi ili kazi imalizike haraka
Ujenzi wa zahanati ya Kwamwande ulianza mwaka 2018 kwa nguvu za wananchi ambapo michango ya wananchi ni shilingi milioni 20,310,100 waliojenga mpaka hatua ya upauaji, shilingi 4,800,000 ni thamani ya ya mabati 150 kutoka Mfuko wa jimbo,shilingi 450,000 ni thamani ya tripu tatu za mchanga kutoka kwa mzabuni aliyejenga kipande cha barabara kutoka Mafisa hadi Mnazi na shilingi milioni 50 kutoka serikali kuu.
Wajumbe wa kamati hiyo walisema serikali imeunga mkono juhudi za wananchi wa kijiji cha Kwamwande ili kuhakikisha mradi unakamilika mapema na kuleta tija kwa jamii
Mradi wa zahanati ya Kwamwande ambao unatarajiwa kukamilika tarehe 30/04/2024 utakapokamilika utatoa huduma kwa wananchi 10,921 wa vijiji vya Kwamwande na Kwastemba
Walisema kamati hiyo itatembelea tena mradi huo tarehe 14/05/2024 ili kuona utekelezaji wa maagizo waliyotoa na kujiridhisha na mwenendo wa ujenzi wa mradi
MODI MNGUMI
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.