Serikali katika kuhakikisha huduma za kijamii ikiwemo afya zinasogezwa karibu na wananchi imeipatia tena Halmashauri ya wilaya Kilindi mkoani Tanga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati katika vijiji vya Elerai na Lulago.
Majengo hayo ya zahanati ya kijiji cha Elerai kilichopo kata ya Kibirashi na Lulago kilichopo kata ya Lwande yalianza kujengwa kwa kutumia nguvu za wananchi na serikali imetoa kiasi hicho cha fedha ili kuunga mkono jitihada za wananchi wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndugu Gracian Makota alisema fedha hizo zitasaidia wananchi hao na Halmashauri nzima kuendelea kuboresha miundombinu ya afya na kuisaidia jamii hususani wakina mama wajawazito na watoto wanaotaabika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mkurugenzi Makota ameishukuru serikali inayoongozwa na Mh:Rais Dk Samia suluhu Hassan kwa namna ambavyo imedhamiria kwa vitendo kutatua changamoto za wananchi kwa wake.
Wakazi wa kijiji cha Elerai wanapata huduma za afya katika zahanati ya Kibirashi ambayo ipo umbali wa kilomita 5 ambapo wakazi wa kijiji cha Lulago wanapata huduma katika zahanati ya Kwadundwa iliyopo umbali wa kilomita 8 ambapo wakati wa mvua wakazi wa kijiji cha Lulago huwawia vigumu kupita katika njia yao ambayo ina miinuko mikali kutokana na jiografia yao ya miinuko.
Tayari serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati 6 zikiwemo Kwamfyomi,Mmbogo,Mnkonde,Mabalanga,Kwamaligwa na Misufini.
Modi Mngumi-Kilindi
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.