Serikali imeipatia Halmashauri ya wilaya Kilindi mitungi ya gesi 31 kwa ajili ya hospitali ya wilaya na kituo cha Afya Songe
Mfamasia wa Halmashauri bibi Mariamu Abubakar alisema katika mitungi hiyo mitungi hospitali ya wilaya imepatiwa mikubwa 28,ambapo kati yake mikubwa ni 23 na midogo ni 5 .
Alisema kituo cha Afya Songe kimepatiwa mitungi mikubwa 3 na kuongeza kuwa mitungi yote 31 ina flow meter zake
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitekeleza kwa vitendo ahadi za kuhakikisha huduma za kijamii ikiwemo afya inaboreshwa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)
Serikali katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya katika ujenzi huo wa hospiatali ya wilaya imeshatoa milioni 90 kwa jili ya ujenzi wa nyumba ya Madaktari ambayo itaishi familia 3,milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura na bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la wazazi (Maternity complex)
Wananchi wa wilaya Kilindi wameipongeza serikali yao kwa namna ambavyo ilivyodhamiria kwa vitendo kuboresha miundombinu ya huduma za afya wilayani kwao
Modi Mngumi
Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.